TUZO ZA FILAMU ZA NYUKA (NYUKA FILM AWARDS)

#
#

MUKTASARI TUZO LA FILAMU ZA NYUKA “NYUKA FILM AWARDS” (NYUMANI KISWAHILI AWADS)

Tuzo maalumu zilizobuniwa mahususi kuwatunza watengeneza filamu za Kiswahili pamoja na wadau wake popote Duniani bila kujali Utaifa wao ili kuienzi na kuikuza Lugha adhimu ya Kiswahili kupitia Sanaa.


Baada ya kupitia michakato mbalimbali washindi watatunzwa katika Usiku maalumu utakaoandaliwa na waandaaji.


Filamu ama watengeneza filamu wanaoruhusiwa kushiriki ni wale waliotengeneza filamu hizo kwa Lugha ya Kiswahili. Baada ya kupitia michakato mbalimbali washindi watatunzwa katika Usiku maalumu utakaoandaliwa na waandaaji.


HALIKADHALIKA kupitia shindano maalumu la uandishi wa Miswada mashuleni ili kukuza vipaji vya kizazi kijacho, Tuzo hizi zitakuwa na mfuko maalumu wa kuwasaidia wasanii wachanga walioko katika shule za msingi mbalimbali katika kuboresha mazingira yao kielimu na kujaribu kupunguza vikwazo mbalimbali vinavyowakabili katika kuendeleza vipaji vyao.


Kupitia Tuzo hizi tunaimani thamani ya Lugha adhimu ya Kiswahili itaongezeka kwani zitakuwa ni ushawishi mkubwa kwa watengeneza filamu Duniani hasa bara la Afrika kutengeneza filamu za Kiswahili hivyo kupelekea kuongeza idadi ya watu wanaozungumza Lugha ya Kiswahili Duniani.